Zaidi ya watu 250 wauawa na kujeruhiwa kwenye shambulizi la Israel dhidi ya hospitali katika Ukanda wa Gaza
2024-03-20 08:39:33| cri


Ofisi ya habari inayosimamiwa na kundi la Hamas jana imetoa taarifa ikisema, zaidi ya watu 250 wameuawa na kujeruhiwa kwenye shambulizi la Israel dhidi ya hospitali ya Shifa kwenye Ukanda wa Gaza.

Taarifa hiyo imesema, kwenye shambulio hilo, wanajeshi wa Israel walifyatua risasi na makombora kwa wagonjwa, watu waliokimbia makazi yao na raia, na kusababisha majeraha na vifo vya wapalestina zaidi ya 250, huku baadhi ya vifaa vya hospitali hiyo vikiteketezwa. 

Taarifa hiyo haikubainisha idadi kamili ya vifo vya watu kwenye shambulio hilo.