Kampuni ya China kujenga uwanja wa kisasa wa soka kaskazini mwa Tanzania
2024-03-20 08:32:55| CRI

Kampuni ya Uhandisi na Ujenzi wa Reli ya China (CRCEG) imesaini makubaliano na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya nchini Tanzania kujenga uwanja wa soka mjini Arusha, Tanzania, kwa ajili ya mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2027.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Wizara hiyo Damas Ndumbaro amesema, utakapokamilika, uwanja huo sio tu utatumika kwa soka, bali pia utatumika kwa shughuli za kibiashara na hafla rasmi za kiserikali.

Mhandisi mkuu wa kampuni ya Uhandisi na Ujenzi wa Reli ya China kanda ya Afrika Mashariki Zhou Zejun amesema, usanifu wa uwanja huo umetokana na madini ya Tanzanite na Mlima Kilimanjaro, huku rangi yake ikitokana na rangi zilizopo katika bendera ya Tanzania.

Tanzania itaungana na Kenya na Uganda kuwa wenyeji wa mashindano ya AFCON ya mwaka 2027.