Bustani ya viwanda iliyojengwa na China nchini Ethiopia yaingiza dola za Marekani milioni 20 ndani ya miezi sita
2024-03-20 08:33:42| CRI

Serikali ya Ethiopia imeingiza dola za Marekani milioni 20 kutokana na mauzo ya bidhaa ndani ya miezi sita kupitia bidhaa zilizozalishwa katika Bustani ya Viwanda ya Hawassa iliyojengwa na China.

Shirika la Habari la Ethiopia limemnukuu meneja mkuu wa Bustani hiyo, Mathiwos Ashenafi akisema, Bustani hiyo inatarajia kuingiza dola za Marekani milioni 44 kutokana na mauzo ya bidhaa zinazozalishwa na wazalishaji walio ndani ya eneo hilo katika mwaka wa fedha wa 2023/2024, ulioanza mwezi Julai mwaka jana.

Bustani hiyo iliyopo kusini mwa mji wa Hawassa, kusini mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, inachukuliwa kama kituo kinachoongoza kwa wazalishaji wa kigeni nchini humo, na inajihusisha na bidhaa za vitambaa na nguo.