Mapato kutokana na mauzo ya nje ya Uganda yapungua kwa asilimia 8.3 katika mwezi Januari
2024-03-20 09:58:49| cri

Wizara ya Mipango ya Kifedha na Maendeleo ya Kiuchumi ya Uganda imesema kwenye ripoti yake ya kila mwezi iliyotolewa Machi 18, kuwa katika mwezi Januari 2024, Uganda ilisafirisha bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 565.40 nje ya nchi, ambazo ni pungufu ya asilimia 8.3 ikilinganishwa na dola za kimarekani milioni 616.36 za mwezi uliopita.

Hata hivyo, kwa upande mwingine, Wizara imesema ikilinganishwa na mwezi huo huo mwaka jana, mauzo ya bidhaa nje ya nchi yaliongezeka kwa asilimia 34.1 kutoka dola za kimarekani milioni 421.55 za mwezi Januari 2023. Hii ilichangiwa na kuongezeka kwa mapato ya mauzo ya dhahabu, kahawa na uuzaji tena nje wa mafuta.