Chakula kilichotolewa na serikali ya China kwa Ukanda wa Gaza wa Palestina kupitia Misri kuwasili Port Said nchini Misri
2024-03-20 11:05:21| cri

Habari kutoka Ubalozi wa China nchini Misri zinasema ili kupunguza changamoto ya hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, serikali ya China inaendelea kutoa msaada kwa Palestina kadri inavyoweza. China imetoa msaada wa fedha taslimu na kutoa shehena mbili za chakula, dawa, vifaa tiba na vifaa vingine vinavyohitajika kwa Ukanda wa Gaza kupitia Misri.

Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, China imezidisha juhudi zake za kutoa chakula kwa Ukanda wa Gaza. Machi 28, msaada wa mchele wa China kwa Palestina utawasili Port Said, nchini Misri, na kusafirishwa hadi Gaza kupitia kivuko cha Rafah.