Tanzania kujenga uwanja wa AFCON wenye thamani ya Sh286 bilioni mjini Arusha
2024-03-20 09:58:18| cri

Serikali ya Tanzania imetenga Sh286 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa soka Mkoani Arusha, utakaopewa jina la Samia Suluhu Hassan, kwa heshima ya Rais aliyeko madarakani. Uwanja huo utajengwa na Kampuni ya Uhandisi wa reli ya China.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Dk. Damas Ndumbaro ametoa taarifa hiyo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa uwanja huo. Waziri Ndumbaro amesema serikali itahakikisha uwanja huo unajengwa na kukamilika kama ilivyopangwa, kabla ya Tanzania kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.