Maofisa wa China na Ethiopia wapongeza nafasi ya BRI katika maendeleo ya Ethiopia
2024-03-21 08:38:33| CRI

Maofisa kutoka Ethiopia na China wamepongeza Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) kutokana na nafasi yake muhimu katika kuboresha maendeleo ya uchumi na jamii nchini Ethiopia na sehemu nyingine duniani.

Wamesema hayo katika kongamano la BRI lililofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, na kuhudhuriwa na maofisa 50 wa ngazi ya juu wa Ethiopia na China, wanafunzi wa Ethiopia waliosoma nchini China, wasomi na wadau wengine wa maendeleo.

Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Mashariki ya Kati, Asia na Pasific katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia Gebeyehu Ganga ameeleza mageuzi ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013 na kuwa jukwaa la kimataifa la ushirikiano wa kimataifa ulio wazi, jumuishi na wa kunufaishana.

Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Ufunguaji Mpango wa Kikanda katika Tume ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China, Xu Jianping amesisitiza matokeo ya ushirikiano na China chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja nchini Ethiopia, na kurejea tena ahadi ya China ya kutekeleza ushirikiano wa ngazi ya juu wa Pendekezo hilo katika muongo wake wa pili.