Xi Jinping atoa pongezi kwa njia ya simu kwa Bw. Prabowo kuchaguliwa kuwa rais wa Indonesia
2024-03-21 11:12:35| cri

Rais Xi Jinping wa China amempongeza Bw. Prabowo Subianto kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Indonesia.

Rais Xi amesema China na Indonesia ni marafiki wakubwa na majirani wema. Kutokana na juhudi za pande mbili, maendeleo ya uhusiano kati ya nchi mbili yameingia katika njia ya kasi, maelewano ya kisiasa yanaimarika siku hadi siku, kuunganishwa kwa mikakati ya maendeleo kati ya nchi hizo mbili kunazidishwa, mafanikio mengi ya ushirikiano wa kunufaishana yamepatikana, huku pande mbili zikifungua ukurasa mpya wa kujenga jumuiya ya China na Indonesia yenye mustakbali wa pamoja .

Rais Xi pia amesema anatilia maanani maendeleo ya uhusiano kati ya China na Indonesia, akitarajia kushirikiana na Bw. Prabowo katika kuongoza ujenzi wa jumuiya ya nchi mbili yenye mustakabali wa pamoja upate maendeleo zaidi, kujenga mfano wa kuigwa wa nchi kubwa zinazoendelea kushirikiana na kutafuta maendeleo kwa pamoja, ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili na kutia msukumo mkubwa kwa utulivu na ustawi wa kanda na dunia nzima.