Kama ilivyotegemewa, baada ya Baraza la Kutunga Sheria la mkoa wa Hong Kong kupitisha kwa kauli moja "Marekebisho ya Sheria ya Usalama wa taifa" tarehe 19 na kukamilisha kwa mafanikio Kifungu cha 23 cha Sheria ya Msingi ya Hong Kong. Baadhi ya watu katika nchi za Magharibi, ikiwa ni pamoja na Baraza la Ulaya, na Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo wa Uingereza Bw. David Cameron walishambulia kanuni za usalama wa taifa za Hong Kong kuongeza mmomonyoko wa uhuru na kuuliza maswali kuhusu mazingira ya biashara ya Hong Kong.
Kwa upande wa maudhui, kulinda haki za binadamu kunatiliwa maanani kwenye kila sehemu ya kanuni za usalama wa taifa za Hong Kong. Kanuni zinakuweka kuheshimu na kulinda haki za binadamu kuwa kanuni muhimu, na kulinda haki na uhuru mbalimbali ulioainishwa katika Sheria ya Msingi, na kanuni husika za Mikataba ya Kimataifa zinazofaa kutekelezwa mkoani Hong Kong zitaendelea kufanya kazi. Kwa hiyo inaonekana wazi kuwa sheria hiyo mpya inalenga kupambana na wahalifu wachache wanaohujumu usalama wa taifa. Kwa wakazi wengi wa Hong Kong na wawekezaji wa kimataifa, sheria hiyo ni mlinzi anayelinda haki na uhuru wao, na usalama wa mali na uwekezaji.