Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amesisitiza kuwa China ni mshirika wa kutegemeka wa ushirikiano kwa Madagascar.
Rais Rajoelina amesema hayo alipopokea hati ya utambulisho iliyowasilishwa na balozi mpya wa China nchini Madagascar Ji Ping. Amesema Madagascar inaweka mkazo mkubwa katika kukuza uhusiano na China, na inaishukuru China kwa mchango wake uliotolewa kwa maendeleo ya Madagascar.
Ji Ping amesema chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wa nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Madagascar umepiga hatua madhubuti, na ushirikiano wa kiutendaji kati ya pande hizo mbili umepata matunda makubwa. Pia amesisitiza kuwa China inapenda kuwa mwenzi wa Madagascar katika njia ya kujiendeleza na kutimiza ustawi, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na kuweka mustakabali mzuri kwa ajili ya watu wa nchi hizo mbili.