Rais Xi Jinping asisitiza kuhimiza maendeleo ya maeneo ya kati ya China
2024-03-21 10:57:33| cri

Rais Xi Jinping wa China alipoongoza mkutano unaohusu kuhimiza maendeleo ya maeneo ya kati ya China mjini Changsha mkoani Hunan tarehe 20, alisisitiza kuwa maeneo ya kati ni maeneo muhimu ya uzalishaji wa nafaka, malighafi ya nishati, utengenezaji wa mashine za kisasa na viwanda vyenye teknolojia ya juu, pia ni kitovu muhimu cha uchukuzi. Amesema sera mbalimbali za kuhimiza maendeleo na ufufuaji wa maeneo hayo, ni lazima zitekelezwe kihalisi.

Rais Xi pia amesema ni muhimu kuongoza uvumbuzi wa viwanda kwa uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia na kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji, na kutekeleza kwa kina miradi ya kuboresha teknolojia kuu na kuboresha vifaa kwenye viwanda vya uzalishaji wa bidhaa na kuhimiza viwanda hivyo kupata maendeleo ya hali ya juu.