WFP yasema watu takriban milioni 28 Sudan na nchi za karibu wanakumbwa na uhaba wa chakula
2024-03-21 10:59:54| cri

Naibu mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Carl Skau tarehe 20 alipotangaza taarifa ya hali ya Sudan kwa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa, alisema mapambano nchini Sudan yanaleta msukosuko zaidi wa chakula kote duniani. Watu takriban milioni 28 walioko Sudan na nchi za karibu wanakumbwa na uhaba mkubwa wa chakula, ikiwa ni pamoja na watu takriban milioni 18 nchini Sudan, watu takriban milioni 7 Sudan Kusini, na watu takriban milioni 3 nchini Chad.

Amesema hali ya uhaba wa chakula nchini Sudan itakuwa mbaya zaidi katika wiki kadhaa zijazo, kama jumuiya ya kimataifa haitachukua hatua za dharura, pengine Sudan itatumbukia kwenye msukosuko wa chakula. Amezihimiza pande zote zinazopambana nchini Sudan zihakikishe msaada wa kibinadamu unafika kwenye sehemu mbalimbali nchini Sudan bila vizuizi.