Uganda yashuhudia ongezeko la asilimia 13.4 kwenye miamala kutoka nje
2024-03-21 22:57:58| cri

Uganda imeshuhudia ukuaji wa asilimia 13.4 kwenye malipo ya binafsi katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, kuishia Januari 2024. Hii ina maana kwamba wapokeaji wa fedha hizo nchini Uganda walisaidiwa kukidhi mahitaji yao ya kaya katika kukabiliana na gharama kubwa za maisha.

Mkurugenzi mtendaji wa utafiti katika Benki ya Uganda Bw. Adam Mugume, amesema mialama hiyo binafsi, ambayo kwa kawaida inaitwa miamala ya wafanyakazi, ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.417 katika kipindi cha miezi 12 hadi Januari 2024, kutoka dola za kimarekani bilioni 1.250 katika kipindi kama hicho hadi Januari 2023, ukiwa ni ukuaji wa takriban asilimia 13.4.

Duniani kwa sasa fedha zinazotumwa kutoka nje ya nchi ziliendelea kuwa chanzo muhimu cha mapato katika mwaka wa 2023, ikilinganishwa na uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni na misaada rasmi ya maendeleo.

Bw. Mugume amesema chanzo kikuu cha fedha hizo ni kutoka Mashariki ya Kati, Ulaya, Amerika na Afrika.