Rais Samia awa mwenyeji wa mkutano kutafuta mafungamano zaidi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
2024-03-21 10:59:16| cri

Marais wa nchi za Afrika Mashariki Samia Suluhu wa Tanzania, William Ruto wa Kenya na Yoweri Museveni wa Uganda wamekutana mjini Zanzibar kujadili masuala yanayohusu na mafungamano ya Afrika Mashariki, hasa kuhusu haja ya kuharakisha ushiriki wa umma kuhusu mtindo wa Shirikisho la Kisiasa la Jumuiya hiyo.

Kenya, Uganda na Tanzania zilianzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya uhuru, lakini baada ya kupitia changamoto kadhaa jumuiya hiyo imepanuka kufikia wanachama wanane wa sasa.

Viongozi hao watatu walikutana katika mkutano ambao haukutangazwa, na ajenda ya mkutano kwa kiasi kikubwa haikuwa wazi. Ikulu ya Tanzania imesema mazungumzo ya viongozi hao watatu hao yaligusa masuala ya mafungamano ya Afrika Mashariki, hasa kuhusu haja ya kuharakisha kuwashirikisha wa wananchi katika muundo wa Shirikisho.