Uhusiano kati ya China na Australia unawezaje “kutorudi nyuma”?
2024-03-22 11:33:41| cri

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 10 tangu China na Australia zianzishe uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa  pande zote. Ziara ya kiserikali iliyofanywa na waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi mwezi Machi nchini Australia inachukuliwa kama ishara ya kupungua kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili.

Serikali ya zamani ya Australia ilikuwa “mtetezi wa mstari wa mbele” wa Marekani katika kuzuia maendeleo ya China ikifuata sera zisizofaa dhidi ya China, ambazo zilisababisha uhusiano kati ya Australia na China kudhoofika. Hali hiyo haikubadilika hadi serikali ya sasa kilipoingia madarakani mwezi Mei mwaka 2022 ambapo ikirekebisha sera yake kuhusu China na uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukaanza kuboreshwa. Mwezi Novemba wa mwaka huo, rais Xi Jinping wa China alikutana na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese wakati wakihudhuria Mkutano wa Viongozi wa kundi la G20 na kufikia maafikiano muhimu ya kisiasa juu ya kuharakisha uboreshaji wa uhusiano wa nchi hizo mbili. Mwezi Novemba mwaka 2023, waziri mkuu Albanese alifanya ziara ya kitaifa nchini China, na kuwa ziara ya kwanza baada ya miaka saba kwa Waziri Mkuu wa Australia nchini China.

Vyombo vya habari vya Australia vimesema katika ziara hiyo ya Bw. Wang Yi, China na Australia zilifanya mikutano mingi, ambapo China ilieleza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili sasa umerejeshwa kwenye njia sahihi na haupaswi kurudi nyuma huku Australia pia ikisisitiza nchi hizo mbili zinatakiwa kutafuta maslahi ya pamoja kadri iwezekanavyo.

Wachambuzi wamesema Australia ikitaka kupata maendeleo ya pamoja na China, lazima ibadilishe kwanza sera yake ya “kuifuata Marekani katika kuzuia maendeleo ya China”, na nchi hizo mbili zinahitaji kufanya juhudi katika pande zifuatazo ili uhusiano wao usirudi nyuma:

Kwanza, ni kuheshimiana na kushughulikia tofauti zao kwa busara. Australia inatakiwa kuheshimu maslahi na masuala makuu yanayofuatiliwa na China. Waziri mkuu Albanese amesisitiza kuwa Australia siku zote inafuata sera ya “China Moja”, ambayo ni msimamo unaoendelea kushikiliwa. Licha ya hayo, maendeleo ya uhusiano kati ya China na Australia yako katika msingi wa kujitegemea na kujiamulia. Australia ni mshirika wa Marekani, pia ni mshirika wa China, na muhimu zaidi ni nchi huru. China inasisitiza kwamba maendeleo ya uhusiano kati ya China na Australia hayalengi upande wa tatu, wala hayapaswi kuathiriwa au kuingiliwa na upande wa tatu. Aidha, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Australia ni msukumo mkubwa zaidi kwa maendeleo ya uhusiano wao. China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Australia kwa miaka 15 mfululizo. Kutokana na kuboreshwa kwa uhusiano wa kisiasa kati ya nchi hizo mbili, ushirikiano wa kibiashara kati yao unatarajiwa kuendelezwa vizuri zaidi bila vizuizi.