Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jana imesema kuwa, inatoa mafunzo kwa maofisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuhusu mafungamano ya kikanda, itifaki ya umoja wa forodha, na wazo la mfumo wa kisheria na mchakato wa kituo kimoja cha mpaka.
Taarifa iliyotolewa na EAC imesema, mafunzo hayo ya siku tano yaliyofanyika huko Kampala, mji mkuu wa Uganda, yameshirikisha maofisa waandamizi kutoka wizara mbalimbali za DRC.