Baraza la usalama la UM latoa taarifa juu ya hali ya Haiti
2024-03-22 14:25:31| cri

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 21 Machi lilitoa taarifa likilaani mashambulizi na vurugu zilizotokea nchini Haiti. Taarifa hiyo imeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu usafirishaji haramu wa silaha nchini Haiti, na kusema kuwa nchi wanachama zina wajibu wa kuzuia usafirishaji wa silaha kwenda nchini Haiti kwa mujibu wa azimio husika.

Taarifa hiyo imesema usafirishaji haramu wa silaha nchini Haiti ni sababu ya kimsingi ya machafuko na vurugu. Taarifa pia imehimiza jumuiya ya kimataifa iwaunge mkono polisi wa Haiti, na kutuma kwa haraka ujumbe wa kimataifa wa msaada wa kulinda usalama ili kuisaidia Haiti kurejesha utaratibu wa jamii.