Rais Macron aunga mkono 'suluhisho kwa njia ya mazungumzo' kutatua mgogoro kati ya DRC na Rwanda
2024-03-22 14:24:17| cri

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema anaunga mkono azimio la kisiasa la kutatua mgogoro kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ikulu ya Elysee ilisema katika taarifa yake.

Jumatano ya Machi 20, Rais Macron alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Joao Lourenço wa Angola, ambaye ni mpatanishi wa nchi hizo mbili chini ya mchakato wa Luanda unaoungwa mkono na Umoja wa Afrika.

Mchakato wa Luanda, ni mpango wa Mkutano wa Kimataifa wa Eneo la Maziwa Makuu (ICGLR) ambao ulianzishwa katikati ya 2022 ili kutatua changamoto ya kidiplomasia iliyotokana na mgogoro kati ya serikali ya DRC na waasi wa kundi la M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC.