Watu 42 wauawa katika mapigano ya kikabila nchini Chad
2024-03-22 08:38:23| CRI

Wizara ya Usalama wa Umma ya Chad imetoa taarifa ikisema, watu wasiopungua 42 wameuawa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea kati ya jamii za Mouro na Birgut katika Jimbo la Quaddai, mashariki mwa Chad.

Wizara hiyo imesema kijiji kimoja kilichomwa moto katika mapigano hayo na watu 175 wamekamatwa, lakini haikutaja chanzo cha mapambano hayo.

Mapambano kati ya wakulima na wafugaji wa kuhamahama yanatokea mara kwa mara katika eneo la mashariki mwa Chad, na hali imekuwa mbaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni kutokana na ukame na ongezeko la idadi ya watu.