China inafanya juhudi ya kuimarisha nafasi yake ya mwekezaji mkubwa wa kigeni nchini Tanzania
2024-03-22 14:27:36| cri

China inataka kuimarisha nafasi yake ya mwekezaji mkuu nchini Tanzania, wakati takriban makampuni 60 ya China yamejipanga kutafuta fursa za uwekezaji nchini Tanzania.

Hadi kufikia Oktoba 2022, China ilichangia miradi 1,098 ya uwekezaji yenye thamani ya dola bilioni 9.6 nchini Tanzania, na ajira 131,718 zimetolewa kupitia miradi hiyo. China inafuatiwa na Uingereza na Marekani kwenye nyanja hiyo.

Ujio unaotarajiwa wa wawakilishi wa kampuni 60 za China Machi 27 kwa ajili ya kongamano la uwekezaji kati ya China na Tanzania, unaashiria kuwa huenda itadumisha nafasi yake ya mwekezaji mkuu nchini Tanzania.