Tanzania mbioni kutumia umeme wa jotoardhi
2024-03-22 14:28:09| cri

Tanzania iko mbioni kuondokana na changamoto ya kukatika kwa umeme kufuatia kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ya Uendelezaji Jotoardhi Ardhi (TGDC) kuja na mpango wa kuviongezea nguvu vituo mbadala hasa 50 vilivyopo katika mikoa 16 nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa TGDC, Mhandisi Mathew Mwangomba amebainisha hayo kwenye mkutano uliowakutanisha wanasayansi wabobevu kutoka Marekani, New Zealand, Japan, Iceland, Kenya, Rwanda na Ethiopia.

Lengo la mkutano huo ni kujadili na kupata mapendekezo ya namna bora ya kuanza uchimbaji wa nishati ya jotoardhi katika Mradi wa Ngozi uliopo Wilaya ya Mbeya ambao kipindi cha kwanza utazalisha megawati 30 ifikapo mwaka 2025, lengo likiwa ni kuzalisha megawati 70.