Makao makuu ya Afrika CDC yapongezwa kama matokeo halisi ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja
2024-03-22 08:36:34| CRI

Ujumbe wa wasomi na maofisa kutoka China umesifu jengo la makao makuu ya Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa Afrika (Africa CDC) nchini Ethiopia kama mfano halisi wa ushirikiano wa China na Afrika chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI).

Pongezi hizo zimetolewa wakati ujumbe wa China unaojumuisha wasomi kutoka Chuo Kikuu cha Beijing, maofisa wa serikali ya China na wadau wengine kutembelea makao makuu ya Africa CDC mjini Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia.

Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC Jean Kaseya amesifu uungaji mkono wa China katika kuwezesha Kituo hicho kutimiza majukumu yake kupitia ujenzi wa uwezo na uungaji mkono wa kiufundi.

Amesema jengo hilo la makao makuu pamoja na maabara zinaiwezesha Afrika na Africa CDC kutimiza majukumu yake katika ngazi ya juu zaidi.