Baraza kuu la UM latangaza mwaka 2025 kuwa ni mwaka wa amani na uaminifu wa kimataifa
2024-03-23 22:25:55| cri

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 21 lilipitisha azimio na kutangaza mwaka 2025 kuwa ni mwaka wa amani na uaminifu wa kimataifa.

Azimio hilo limeihimiza jumuiya ya kimataifa itatue migogoro kwa njia ya mazungumzo shirikishi, kuhakikisha kuimarisha amani na uaminifu kwenye mahusiano ya kimataifa, na kuvifanya viwe sehemu ya maadili katika kuhimiza maendeleo endelevu, amani, usalama na haki za binadamu.

Baraza hilo tarehe 21 pia lilipitisha azimio na kutangaza kuwa tarehe 15 Novemba kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kuzuia na kupambana na uhalifu wa kuvuka mpaka, ili kuongeza ufahamu wa umma kuhusu tishio linaloletwa na uhalifu huo, na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wa pande husika.