Kenya kuunganisha HELB na KUCCPS kuwa taasisi moja
2024-03-25 22:56:18| cri

Wizara ya Elimu ya Kenya imewasilisha muswada wa sheria ya kuunganisha Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB) na Halmashauri ya Kuwateua Wanafunzi Kujiunga na Vyuo Vikuu na Vyuo Anuwai (KUCCPS) nchini humo kuwa taasisi moja.

Muswada huo unapendekeza kuuundwabuniwa kwa Halmashauri ya Ufadhili na Usimamizi wa Elimu Anuwai (TEPFA), ambayo jukumu lake litakuwa kuwasajili wanafunzi katika taasisi za mafunzo anuwaina, kutoa mikopo na ufadhili wa elimu kwa wanafunzi katika taasisi hizo. Pia, Halmashauri hiyo itatoa miundomsingi ya ufadhili kwa taasisi hizo.

Muswada huo tayari umetolewa kwa umma ili kuwapa wananchi nafasi ya kutoa maoni yao.