Sudan Kusini kutumia zao la Gum Arabic wakati mapato yake ya mafuta yakipungua
2024-03-25 08:46:38| CRI

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan Kusini Bw. William Anyuon Kuol, amesema Sudan Kusini inatazamia kuongeza makusanyo ya mapato yasiyotokana na mafuta kwa kuhimiza vyanzo mbalimbali vya uchumi wake, na kutumia maliasili ambazo hadi sasa bado hazijavunwa kama za sekta ya Gum Arabic, matunda na mboga mboga.

Bw. Akuol ameyasema hayo mjini Nimule karibu na mpaka wa Uganda, kuwa katika mkakati mpya wa taifa wa uwekezaji wa Sudan Kusini, wamegundua Gum Arabic kuwa ni bidhaa muhimu inayoweza kuingiza fedha za kigeni, na kupanua vyanzo vyake vya mapato.

Sudan Kusini ambayo bajeti yake inategemea asilimia 95 ya mapato ya mafuta, inakabiliwa na vizuizi vya kusafirisha mafuta yake kupitia Bandari ya Sudan kutokana na mgogoro unaoendelea katika nchi hiyo.