Maoni ya pamoja yaliyofikiwa mjini Beijing yafafanua masuala ya kimsingi ya demokrasia
2024-03-25 13:19:53| cri

Kongamano la 3 la kimataifa la Demokrasia, Thamani ya Pamoja ya Binadamu wote linafanyika hapa Beijing. Zaidi ya wajumbe 200 kutoka nchi na mashirika mbalimbali duniani wamehudhuria kongamano hilo, na wamejadili kwa kina masuala kadhaa yanayofuatiliwa sana yakiwemo demokrasia na usimamizi wa kisasa, akili bandia na mustakabali wa demokrasia, demokrasia kwenye dunia yenye ncha nyingi na usimamizi wa mambo ya kimataifa. Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limetoa tahariri ya maoni ya pamoja yaliyofikiwa mjini Beijing yafafanua masuala ya kimsingi ya demokrasia.

Tahariri hiyo inasema kwenye kongamano hilo, wajumbe hao wamefikia maoni ya pamoja kwamba, lengo la kutekeleza demokrasia ni kuhakikisha na kuzidisha maisha bora ya binadamu wote, hivyo inapaswa kuheshimu haki ya watu wa nchi tofauti kuchagua njia yao ya kujiendeleza, na kupinga vitendo vya kuchochea ufarakanishaji, ubaguzi na kuharibu amani kwa kisingizio cha demokrasia.

Maoni hayo yanakumbusha kwamba watu wenye maoni tofauti kuhusu demokrasia wanaweza kufanya mazungumzo ili kuelewana, na nchi za magharibi hazitafanikiwa kwa kuzilazimisha nchi nyingine kupokea maoni yao.