Somalia yapata mafanikio katika kupambana na Kifua Kikuu
2024-03-25 22:58:01| cri

Somalia imesema imepata maendeleo makubwa katika kutimiza lengo la kimataifa la kuondokana na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) itakapofika mwaka 2030, na kutoa wito kwa uwekezaji zaidi ili kudumisha mafanikio hayo.

Hayo yamesema na meneja wa program ya Kifua Kikuu katika Wizara ya Afya na Huduma za Umma nchini Somalia, Mohamed Jafar wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani. Amesema mradi wa kupambana na TB nchini humo umekabiliana na changamoto mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa usalama na janga la COVID-19, na kuonyesha mafanikio ya asilimia 87 katika tiba.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya vituo vya tiba ya TB nchini Somalia imeongezeka na kufikia vituo 109 mwaka jana kutoka vituo 7 mwaka 1995.