Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi 30 zenye maambukizi makubwa ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).
Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Health Promotion Tanzania (HDT), Dk Peter Bujari wakati wa maadhimisho ya SiIku ya Kifua Kikuu Dunianihapo jana. Amesema maambukizi makubwa ya ugonjwa huo katika nchi hizo 30 yanachangia asilimia 87 ya maambukizi yote duniani.
Amesema takwimu za mwaka 2023 zinaonyesha kuwa, Tanzania ilikuwa na wagonjwa 128,000wa kifua kikuu, na kwamba hadi sasa maambukizi mapya ni 100,000 na wagonjwa 18,000 wamefariki kutokana na ugonjwa huo.