Hivi karibuni Kampuni ya utengenezaji ndege ya Boeing ya nchini Marekani imekutwa na mashitika kufuatia madai ya “kujiua” kwa John Barnett, mfanyakazi mstaafu wa Kampuni hiyo, siku chache baada ya kutoa ushahidi kuhusu masuala ya usalama na utengenezaji wa ndege na ajali mbalimbali za ndege za kampuni hiyo.
Serikali ya Marekani haiwezi kukaa kimya tena. Siku chache zilizopita, waziri wa usafiri wa Marekani Pete Buttigieg na mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Anga Michael G. Whitaker wamekiri kuwepo kwa matatizo ya usimamizi wa ubora wa ndege za Boeing. Lakini wote hawakujibu kuhusu hatua za utatuzi na majukumu ya usimamizi ya serikali, ambayo ni masuala yanayofuatiliwa zaidi na watu.
John Barnett mwenye umri wa miaka 62 aliyehudumia Kampuni ya Boeing kwa zaidi ya miaka 30, alikuwa meneja wa udhibiti wa ubora wa ndege katika kampuni hiyo. Alizungumzia mara kwa mara masuala ya usalama wa utengenezaji wa ndege na mvutano ndani ya kampuni hiyo, na alikutwa amekufa ndani ya lori, na polisi wa Marekani kusema kuwa “alijiua kwa kujipiga risasi”.
Kifo cha Barnett ni sehemu moja tu katika “Mgogoro wa uaminifu” ulioikumba Kampuni ya Boeing, ambayo tokea mwaka huu, imekutwa na matatizo mbalimbali ya usalama. Wachambuzi wanaona kuwa utengenezaji ya Kampuni umekumbwa na matatizo kwa muda mrefu ambayo yanatokana na msisitizo juu ya hisa kuliko ubora, mabadiliko ya mara kwa mara ya wakuu, na ukosefu wa utaratibu wa uwajibikaji. Pia, kukosa kwa usimamizi wa idara husika za serikali ya Marekani ni chanzo cha matatizo ya kampuni ya ndege ya Boeing. Kwa miongo kadhaa, Shirikisho la Usafiri wa Anga (FAA) limekabidhi baadhi ya kazi ya utoaji wa vyeti kwa kampuni za utengenezaji wa ndege ikiwemo Boeing ili kuokoa pesa, hatua ambayo ni kama kuwapa wachezaji madaraka ya waamuzi.
Kwa mtazamo wa Bloomberg na vyombo vingine vya habari vya nchi za nje, ajali mfululizo za ndege za Kampuni ya Boeing ambayo ina ushawishi mkubwa zaidi katika sekta ya usafiri wa ndege duniani, zitaleta athari hasi kwa sekta hiyo.
Usalama wa ndege sio jambo dogo bali unahusiana na usalama wa umma duniani. Pande mbalimbali zinazohusika za Marekani hazipaswi kukwepa uwajibikaji wake kwa matukio hayo yenye mashaka, bali zinatakiwa kujibu kwa udhati wasiwasi wa watu na kutoa maelezo mwafaka kwa dunia.