Polisi wa Kenya wakamata vifaa vya vilipuzi kwenye shambulizi dhidi ya kituo cha kundi la al-Shabab mpakani
2024-03-25 09:13:26| CRI

Polisi wa Kenya wameshambulia kituo kimoja cha kundi la al-Shabab kilichoko katika kaunti ya Garissa, kaskazini mwa nchi hiyo, na kukamata mabomu yaliyotengenezwa kienyeji (IEDs) na vingine.

Polisi wamesema kituo hicho kilikuwa nyumba ya magaidi watatu wenye utaalamu wa kutengeneza mabomu, ambao walikimbia wakiwa na majeraha makubwa baada ya operesheni ya polisi, kwa sasa idara za usalama zinawasaka magaidi hao.

Mamlaka za usalama za Kenya zimetoa wito kwa wakazi wa eneo hilo la mpakani kuripoti washukiwa wowote wa ugaidi ili wachukuliwe hatua kwa ajili ya usalama wa nchi hiyo.