Kongamano la kimataifa la utafiti wa lugha na tamaduni za Afrika la 2024 lafanyika Beijing na Paris
2024-03-25 08:50:00| cri

Kongamano la kimataifa la utafiti wa lugha na tamaduni za Afrika la 2024 linafanyika tarehe 22 na 23 Machi 2024 Beijing na Paris. Kongamano hilo limeandaliwa na Kitivo cha Lugha za Afrika cha Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijng (BFSU), Chuo cha Lugha na Tamaduni za Mashariki cha Ufaransa (INALCO).

Naibu mkuu wa BFSU Jia Dezhong, naibu mkuu wa INALCO Isabelle Konuma, na balozi wa China nchini Jamhuri ya Congo Li Yan wameshiriki kwenye ufunguzi na kutoa hotuba. Wataalamu na wasomi 40 kutoka vyuo vikuu na mashirika ya China, Ufaransa, Sweden, Ujerumani, Ethiopia, Nigeria, Afrika Kusini, Madagascar, Cameroon, Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Congo wameshiriki kwenye kongamano hilo. Umoja wa Vyuo Vikuu vya Lugha za Kigeni Duniani na Taasisi ya Asia na Afrika ya China ni mashirika yaliyotoa uungaji mkono kwenye kongamano hilo.

Naibu mkuu wa BFSU Jia Dezhong alisema, BFSU inadhamiria kujenga chuo kikuu hodari cha lugha za kigeni na chenye sifa ya kipekee duniani, kinachotoa mafunzo ya kiwango cha juu. Kinajitahidi kufanya kazi yake kubwa zaidi katika kufundishana kwa ustaarabu wa dunia. BFSU pia inafanya juhudi katika kuwaandaa watu wenye ujuzi wa lugha na utafiti wa Afrika. Ushirikiano kati ya BFSU na INALCO una historia ndefu, na ushirikiano kati ya BFSU na vyuo vikuu vingi vya Afrika umepata matokeo mengi mazuri.

Balozi wa China nchini Jamhuri ya Congo Li Yan amesema kongamano hilo limeshirikisha wataalamu kutoka China, Ufaransa na Afrika, na linaonyesha sifa ya mawasiliano na mazungumzo ya ustaarabu, na kuonyesha maana ya kina ya jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Naibu mkuu wa INALCO Isabelle Konuma alisisitiza kuwa, vyuo vikuu na taasisi za utafiti zinazoshiriki kwenye kongamano hilo zina uwezekano mkubwa wa ushirikiano katika kuwaandaa wataalamu na kufanya utafiti, mipango mingi zaidi ya ushirikiano inatarajiwa kutekelezwa.

Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya “Mafunzo ya lugha na tamaduni za Afrika chini ya wazo la mawasiliano ya kozi mbalimbali” linatoa jukwaa la mawasiliano ya mafunzo kwa wasomi na walimu wanaofanya utafiti wa lugha na tamaduni za Afrika kote duniani. Wataalamu walioshiriki kwenye mkutano walichangia mawazo yao ya akademia na kufanya mawasiliano. Wasomi wengi wa Afrika walioshiriki kwenye kongamano hili nchini China kwa mara ya kwanza, wamesema jitihada za sekta ya akademia ya China zinahimiza kueneza  lugha na tamaduni za Afrika duniani.