Nyumbani na nje, simulizi za kale na hekaya---Mazungumzo kati ya Gurnah na Mo Yan
2024-03-26 11:03:05| cri

Mshindi wa tuzo ya Nobel ya fasihi Abdulrazak Gurnah aliizuru China kwa mara ya kwanza hivi karibuni, ambako aliwasiliana na waandishi wa fasihi na kujifunza utamaduni katika miji kadhaa, ikiwemo Beijing. Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa ilipiga picha ya video kuhusu shughuli ya “Nyumbani na nje, simulizi za kale na hekaya---Mazungumzo kati ya Gurnah na Mo Yan”, kufanya mahojiano na waandishi hao wawili, na kuandaa kipindi cha “Fasihi ya ndani na nje--- Mazungumzo kati ya Gurnah na Mo Yan.” Katika kipindi hicho  Gurnah ameeleza wazo lake juu ya utamaduni kwa upande wa mgeni, na Mo Yan kueleza utamaduni na ustaarabu wa Afrika Mashariki kama anavyoufahamu.