Uganda yamtangaza kamanda mpya wa kikosi chake katika Tume ya ATMIS
2024-03-26 14:29:16| cri

Jeshi la Uganda limemtangaza kamanda mpya wa kikosi chake katika Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS).

Katika taarifa yake iliyotolewa jana mjini Kampala, Jeshi hilo limesema, Sam Kavuma atachukua nafasi ya Samuel Okiding, ambaye ameteuliwa kuwa makamu wa mkuu wa majeshi ya ulinzi ya Uganda.

Hatua hiyo inakuja baada ya rais wa Uganda, Yoweri Museveni kufanya mabadiliko kadhaa katika jeshi la nchi hiyo, ikiwemo kumteua mtoto wake Muhoozi Kainerugaba kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi ya Uganda.