China yasisitiza kuwa azimio la kusitisha vita ukanda wa Gaza la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lazima litekelezwe
2024-03-26 09:15:07| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amesema azimio la usitishwaji vita huko Gaza lazima litekelezwe.

Balozi Zhang amesema, katika miezi sita iliyopita tangu mgogoro wa Gaza kutokea, raia zaidi ya elfu 32 wa kawaida wameuawa. Kwa wale waliopoteza maisha, azimio hilo limechelewa sana kupitishwa. Lakini kwa mamilioni ya watu wa Gaza ambao bado wamekwama kwenye janga kubwa la kibinadamu lisilowahi kushuhudiwa katika historia, azimio hilo litaweza kuleta matumaini yanayosubiriwa kwa muda mrefu kama litatekelezwa kihalisi na kikamilifu.
Amesema azimio la baraza la usalama lina nguvu ya kulazimisha, China inazitaka pande husika zitekeleze majukumu yaliyowekwa na Katiba ya Umoja wa Mataifa na kuchukua hatua kwa mujibu wa matakwa ya azimio hilo.