Waziri wa mambo ya nje wa Tunisia aahidi kuimarisha ushirikiano na shirika la maendeleo la Umoja wa Afrika
2024-03-26 08:42:44| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa Tunisia Nabil Ammar ameahidi kuimarisha hatua ya pamoja na yenye ufanisi ya Afrika na kuunga mkono taasisi za Umoja wa Afrika.

Akikutana na ofisa mtendaji mkuu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika (AUDA-NEPAD), Nardos Bekele-Thomas,  Bw. Ammar amesistiza ahadi ya Tunisia ya kuimarisha ushirikiano na shirika hilo na nia yake ya kunufaika kutokana na programu na miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo.

Waziri huyo pia amesisitiza umuhimu wa shirika hilo kuhamasisha raslimali ili kuziunga mkono nchi wanachama na mashirika ya kikanda ya Afrika kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na vilevile kutoa huduma za ushauri na msaada wa kiufundi.