Ushirikiano wa BRI waboresha maisha ya Waethiopia
2024-03-26 23:26:07| cri

Wataalamu nchini Ethiopia wamesema, ushirikiano na China chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) umekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya raia wa kawaida wa Ethiopia.

Mtafiti mwandamizi wa diplomasia na masuala ya kimataifa katika Taasisi ya Mambo ya Nje ya Ethiopia, Melaku Mulualem amesema, Ethiopia, ikiwa moja ya nchi zinazoshirikiana na China chini ya BRI imeshuhudia mchango mkubwa wa Pendekezo hilo katika mabadiliko ya kihalisi ya mamilioni ya Waethiopia.

Amesema raia wengi wa Ethiopia wanafanya kazi katika miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya BRI, ikiwemo maeneo ya viwanda, vituo vya treni, ujenzi wa barabara kuu na barabara za mwendokasi, na miradi mingine.