Rais Xi Jinping akutana na Waziri Mkuu wa Dominica
2024-03-26 08:43:35| CRI

Rais Xi Jinping wa China amekutana na Waziri Mkuu wa Dominica Roosevelt Skerrit ambaye yuko ziarani nchini China .

Akiitaja Dominica kuwa nchi muhimu kwenye eneo la Caribbean, na vilevile rafiki na mwenzi mzuri anayeaminika kwa China kwenye eneo hilo, Rais Xi amesema nchi hizo mbili zimeheshimiana na kutendeana kwa usawa tangu uhusiano wa kibalozi kati yao ulipoanzishwa miaka 20 iliyopita.

Rais Xi amesema, China inapenda kushirikiana na Dominica katika kuunganisha mikakati yao ya maendeleo na kubadilisha uhusiano wa kirafiki kuwa nguvu ya msukumo ya ushirikiano wa kunufaishana ili kuzinufaisha zaidi  nchi hizo mbili na watu wake.

Rais Xi ameongeza kuwa China inaikaribisha Dominica kutumia fursa ya maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China ili kupanua ushirikiano kwenye sekta mbalimbali ikiwemo uchumi na biashara, miundombinu, kilimo na huduma za afya, na China itaendelea kutoa msaada kadiri iwezavyo kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Dominica.