AU, TikTok waungana kuwawezesha vijana wa Afrika kuhusu usalama wa kidijitali
2024-03-26 08:59:03| CRI

Umoja wa Afrika (AU) na jukwaa la kushiriki video la TikTok, wametangaza kampeni ya pamoja iitwayo “Safer Together”  ili kuwawezesha vijana wa Afrika kuwa na ujuzi na nyenzo za kutumia mtandao wa internet kwa usalama.

Umoja wa Afrika umesema kwenye taarifa iliyotolewa jumapili, kuwa mpango huo ulizinduliwa kwenye mkutano wa hivi karibuni wa TikTok Safer Internet Summit nchini Ghana, ambao una lengo la kuwawezesha si kama tu vijana wa Afrika bali pia wazazi na waelimishaji kuhusu usalama wa kidijitali.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Wanawake, Jinsia na Vijana katika Tume ya AU, Prudence Ngwenya, amepongeza ushirikiano huo kuwa ni hatua muhimu ya kuwawezesha vijana wa Afrika na kulinda mustakabali wao wa kidijitali.