Siku ya Down Syndrome--“Komesha Fikra Potofu kuhusu Down Syndrome”
2024-03-26 08:29:13| CRI

    Machi 21 kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Down Syndrome. Down Syndrome ni hali ya kuzaliwa nayo ambayo inatokana na kasoro za kijenetiki kwenye mwili wa mtoto. Mtoto mwenye ugonjwa huu anaonekana kuwa mzito kuanzia kujifunza, kutumia mwili wake na hata kiakili kuliko watoto wengine wa kawaida. Hali hii inaweza kuambatana na kasoro tofauti tofauti katika maumbile ya mtoto ikiwemo magonjwa ya moyo, uwezo mdogo wa kusikia au kutosikia kabisa, ugonjwa wa Kisukari na matatizo mengine. Hali hii ya Down Syndrome, maana wataalamu wa afya wanasema huu si ugonjwa, bali ni hali, sasa hali hii ya Down Syndrome imekuwa ikipuuzwa naweza kusema kwa kiasi Fulani, kwa sababu mtoto anapozaliwa na hali hiyo kwa kule kwetu anapewa majina mengi ya kudhalilisha, ikiwemo ndondocha, chizi ama taahira.

    Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku hii inasema “Komesha Fikra Potofu kuhusu Down Syndrome”. Kauli mbiu hii inalenga kuachana na Imani potofu kuhusu tatizo hili na kupinga unyanyapaa, kuwezesha huduma wanazohitaji kama vile mazoezi tiba na kutoa elimu zaidi kwa jamii. Hivyo basi katika kipindi hiki cha Ukumbi wa Wanawake, tutakuwa na mengi ya kujifunza juu ya hali hii ya Down Syndrome.