Togo kupitisha katiba mpya, kuhamia mfumo wa bunge
2024-03-27 08:44:55| CRI

Bunge la Togo limepitisha marekebisho ya katiba ya nchi hiyo na kubadilisha nchi hiyo kutoka mfumo wa urais hadi mfumo wa bunge. Wabunge 89 kati ya 91 walipiga kura kuunga mkono marekebisho mapya ya katiba ya Togo, ambayo yalisitisha kufanyika kwa uchaguzi wa rais.

Kufuatia marekebisho hayo, rais wa jamhuri atachaguliwa na mkutano wa bunge kwa kipindi kimoja cha miaka sita. Hadi kufikia wakati huo, rais atakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano, kinachoweza kuongezwa mara moja, lakini kwa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi.

Nakala ya kikatiba iliyopitishwa imeunda nafasi mpya ya ‘mkuu wa Baraza la Mawaziri,’ aliyechaguliwa kwa muhula wa miaka sita, ambaye atakuwa na mamlaka kubwa katika usimamizi wa masuala ya serikali na atawajibika kwa bunge.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria za Kikatiba Bw.Tchitchao Tchalim, amesema sheria hiyo itakapoanza kutumika, mkuu wa nchi atapokonywa madaraka, na mkuu wa baraza la mawaziri ndio atakuwa mwenye madaraka zaidi.