IGAD: Pembe ya Afrika kupata mvua kubwa hadi mwezi Juni
2024-03-27 08:44:03| CRI

Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa (CPAC) cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya nchi za mashariki mwa Afrika (lGAD), imesema sehemu kubwa ya eneo la Pembe ya Afrika inatazamiwa kuwa na mvua kuliko kawaida kati ya mwezi Aprili na Juni mwaka huu.

Kituo hicho kimesema kwenye utabiri wake wa hivi karibuni kuwa hali ya mvua kuliko kawaida inatazamiwa katika sehemu nyingi za ikweta na kaskazini mwa eneo hilo. Kuna uwekezano mkubwa wa kuwepo kwa mvua kupita kiasi kwenye sehemu ya ikweta na kaskazini mashariki mwa eneo hilo kuanzia Aprili hadi Juni, huku maeneo machache magharibi mwa Ethiopia na magharibi mwa Sudan Kusini yakitazamiwa kuwa kame kuliko kawaida.

Mvua hizo zitakuwa ni mwendelezo wa kipindi cha mvua kubwa katika msimu wa Machi-Mei, ambao umeanza huku mvua hizo zikisababisha vifo na mafuriko katika baadhi ya nchi.