Asilimia kubwa ya wahamiaji wa Afrika wahama ndani ya Afrika
2024-03-27 08:29:58| CRI

Ripoti mpya iliyotolewa Jumanne na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa inasema, asilimia kubwa ya wahamaji wa kimataifa wa Afrika wanahama ndani ya bara hilo.

Ripoti ya pili kuhusu uhamiaji barani Afrika  iliyotolewa kwa pamoja na Umoja wa Afrika na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) mjini Addis Ababa,   imesema uhamiaji barani Afrika ni hali yenye utatanishi, na kuna sababu nyingi zinazowafanya watu   wafanye maamuzi kuhusu uhamiaji ndani au nje ya bara.

Takwimu za ripoti hiyo zinaonesha kuwa watu milioni 25.1, ikiwa ni asilimia 1.9 ya jumla ya watu bilioni 1.3 wanaoishi barani Afrika, wanaishi nje ya nchi walizozaliwa, kiwango ambacho kiko chini ya wastani wa asilimia 3.6 wa duniani mwaka 2020.