Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limefanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu kazi zake mpya zilizotengenezwa kwa teknolojia ya AI, na wanahabari kutoka nchi 26 wameshuhudia jinsi CMG lilivyoeleza hadithi za kimithiolojia kwa teknolojia hiyo.
Kwenye mkutano huo, CMG lilizindua tamthilia fupi za Hadithi za Kimithiolojia za China za lugha mbalimbali zilizotengenezwa kwa teknolojia ya AI. Naibi mhariri mkuu wa CMG Fan Yun ameeleza majaribio ya shirika hilo katika utafiti wa matumizi ya teknolojia ya AI, uvumbuzi wa teknolojia hiyo, na usanifu wa matumizi ya teknolojia hiyo.