Michuano ya Ubingwa wa Dunia wa Mbio za Magari mwaka 2024 kufanyika nchini Kenya
2024-03-27 23:35:01| cri

Michuano ya Ubingwa wa Dunia wa Mbio za Magari (WRC) zinazojulikana kama Safari Rally Kenya inakaribia kufanyika nchini Kenya.

Madereva pamoja na wasaidizi wao wamekagua vifaa vyao na kufanya marekebisho yanayotakiwa kabla ya ukaguzi rasmi wa mwisho kabla ya kuanza kwa mbio hizo mjini Naivasha, kilomita 90 kaskazini magharibi mwa Nairobi.

Michuano ya wiki hii itamalizika Jumapili, na inatarajiwa kuwa michuano yenye changamoto zaidi tangu kuanza tena kwa mashindano hayo mwaka 2021.

Jumla ya washindani 29 wataanza rasmi michuano hiyo Alhamisi.