Chanjo ya malaria mbioni kutumika nchini Tanzania
2024-03-27 14:32:38| cri

Tanzania ipo mbioni kuanza matumizi ya chanjo ya malaria kwa watoto walioko chini ya umri wa miaka mitano baada ya utafiti wa chanjo mbili kukamilika na kuthibishwa na shirika la Afya Duniani (WHO).

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha tatu cha Baraza la Kupambana na Malaria Tanzania, Kaimu Meneja mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria katika Wizara ya Afya, Samwel Lazaro amesema, wizara kupitia mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) wako kwenye hatua za kuhakikisha chanjo hizo zinasajiliwa ili iweze kutumika.

Naye Mtafiti wa Masuala ya Malaria na Mkurugenzi wa Sayansi katika Taasisi ya Afya ya Ifakara Ally Olotu amesema, wamefanya tafiti za chanjo mbili ambazo ni RTSs ambayo walianza kufanyia tafiti mwaka 2014 hadi 2019.