Rais wa China akutana na wageni kutoka Marekani
2024-03-27 19:23:18| cri

Rais Xi Jinping wa China alikutana na wadau wa sekta za biashara, mikakati na taaluma kutoka Marekani leo Jumatano mjini Beijing. Xi alisema mafanikio ya China na Marekani ni fursa ya kila mmoja.Kama pande zote mbili zinachukuliana kama washirika kwa kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na kushirikiana, uhusiano kati ya China na Marekani utakuwa bora.