Sudan Kusini yafungua tena shule huku wimbi la joto likipungua
2024-03-27 09:19:41| CRI

Sudan Kusini imetangaza kufungua tena shule kuanzia tarehe 2 mwezi Aprili huku kiwango cha juu cha joto kutokana na wimbi la joto kikitarajiwa kupungua.

Serikali ilifunga shule zote kwa muda usiojulikana tarehe 16 mwezi huu kwa sababu ya wimbi la joto kali ambalo lilitarajiwa kuendelea kwa wiki mbili. Mawimbi ya joto kali yalisababisha joto kati ya nyuzi joto 41 na nyuzi joto 45 wakati wa mchana na usiku.

Waziri wa elimu wa nchi hiyo Bw. Awut Deng Acuil alisema ufuatiliaji wa wizara ya mazingira na misitu wa hali ya joto ya kila siku nchini Sudan Kusini umeonesha kushuka kwa kasi kwa joto, na utabiri zaidi unasema mawimbi ya joto yatapungua na msimu wa mvua unaotarajiwa utaanza katika wiki zinazofuata.