Kampuni ya Mafuta ya Botswana imetangaza kuwa kampuni za mafuta za kimataifa zitapigwa marufuku kuingiza bidhaa za mafuta nchini humo kuanzia Aprili 1.
Kwa mujibu wa agizo hilo, asilimia 90 ya mafuta yanayoagizwa kutoka nje ya Botswana yataingizwa na Kampuni ya Mafuta ya Botswana, huku asilimia 10 ikiingizwa na kampuni za wazawa.
Mhandisi mkuu wa Idara ya Nishati katika Wizara ya Madini na Nishati, Baruti Regoeng amesema agizo hilo jipya litabadilisha hali ya sekta ya mafuta kudhibitiwa na wageni, na kuleta fursa za uwekezaji kwa kampuni za wazawa.