Ni ishara gani inayotolewa na ziara ya kwanza ya rais wa Nauru nchini China baada kurejeshwa uhusiano wa kibalozi kati ya pande hizo mbili?
2024-03-27 14:34:30| cri

Rais wa Nauru David Adeang amefanya ziara nchini China tangu tarehe 24 hadi 29 mwezi huu. Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Nauru kufanya ziara nchini China tangu uhusiano wa kibalozi kati ya pande hizo mbili uanzishwe mwezi Januari mwaka huu.

Katika mazungumzo kati ya marais wa China na Nauru yaliyofanyika mchana wa tarehe 25 Machi, rais Xi alisema urafiki haujalishi mpangilio wa nafasi, na mara tu utakapoanzishwa utakuwa na mustakabali mzuri, na kwamba ushirikiano haujalishi mkubwa au mdogo, ukifanyika kwa udhati utapata matunda mazuri.

Kwa upande wake Rais Adeang amesema, Nauru inaisifu China kwa kushikilia kithabiti usawa kati ya nchi zote, bila ya kujali ni kubwa au ndogo, na kwamba inapenda kufuata sera ya kuwepo kwa China moja na kuimarisha ushirikiano na China. Mazungumzo kati ya marais hao wawili yameashiria mambo mengi. 

Idadi ya watu wa China ni zaidi ya bilioni 1.4 huku ile ya Nauru ni zaidi ya elfu 10 tu. Heshima kubwa iliyopewa na China kwa Nauru si kama tu imeonesha ukarimu wa China ikiwa nchi yenye desturi ya uadilifu, bali pia imeonesha njia ya kibalozi ya China ya kuzitendea nchi nyingine kwa usawa. Rais Xi amemwambia rais Adeang kuwa, China ina marafiki wengi katika Pasifiki ya Kusini, na sasa inafurahi sana kwa kuwa na Nauru kama rafiki mpya, na urafiki huu wenye usawa ni kitu ambacho kinathaminiwa na Nauru, ikiwa nchi ya kisiwa katika Pasifiki.

Tangu kurejeshwa kwa uhusiano wa kibalozi mwezi Januari hadi kufanyika kwa ziara ya rais wa Nauru nchini China mwezi Machi, sera ya kuwepo kwa China moja ni msingi wa kukua kwa uhusiano kati ya China na Nauru. Pande hizo mbili zimethibitisha tena kanuni hiyo wakati wa ziara ya rais Adeang nchini China, ambapo si kama tu rais Adeang ameutaja “urejeshwaji wa uhusiano wa kibalozi na China” kuwa ni “kusimama katika upande sahihi wa historia”, bali pia amesema “huu ni mnara muhimu katika uhusiano kati ya Nauru na China”, hatua ambayo imeonesha kwa mara nyingine tena kuwa, sera ya kuwepo kwa China moja ambayo ilithibitishwa katika Azimio No. 2758 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1971, vilevile imekubaliwa na dunia nzima. Mbali na hayo, ziara hiyo ya rais Adeang pia ni ukumbusho kwa Taiwan kuwa, sera ya kuwepo kwa China moja ni mwenendo mkuu ambao unafuata matakwa ya watu, na Taiwan inatakiwa kufanya maamuzi sahihi mapema.

Wakati wa ziara ya Rais Adeang nchini China, Nauru imekuwa nchi mpya iliyosaini nyaraka za ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Kutokana na taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi hizo mbili, China inapenda kuunganisha mikakati yake ya maendeleo na Nauru katika kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kupanua ushirikiano wa kiutendaji katika sekta za biashara na uwekezaji, ujenzi wa miundombinu, mambo ya kilimo na uvuvi, uendelezaji wa kisayansi wa madini, na uhifadhi wa mazingira, pia inapenda kutoa misaada kadiri iwezavyo kwa Nauru katika hatua yake ya kutafuta maendeleo endelevu kwa kujitegemea.

Wachambuzi wanaona kuwa, pendekezo la kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” limekuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi katika nchi mbalimbali za kanda ya Pasifiki, na mafanikio hayo yameshuhudiwa na serikali na wananchi wa Nauru.

Baada ya pendekezo la kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kati ya China na Nauru kutekelezwa, pande hizo mbili zitafanya ushirikiano katika sekta mbalimblai zikiwemo kusafisha maji ya bahari, nishati ya kijani na maendeleo endelevu, ambao utakuwa msukumo mpya katika kuimarisha uhusiano kati ya pande hizo mbili.