Bassirou Diomaye Faye athibitishwa kuwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa Senegal
2024-03-28 08:52:15| CRI

Mgombea wa muungano wa upinzani wa Senegal Bw. Bassirou Diomaye Faye, ameshinda uchaguzi mkuu wa Senegal kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Kuhesabu Kura Jumatano wiki hii.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Amady Diouf amesema kwenye mkutano na wanahabari kwamba Bw. Faye amepata kura milioni 2,43 ambazo ni asilimia 54.28 ya jumla ya kura.  Waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 61.30 ya watu waliojiandikisha kupiga kura. Mpinzani wake mkuu kutoka muungano tawala Amadou Ba amepata asilimia 35.79 ya kura zote.